Wednesday, November 22, 2023

HALI YA MGONJWA KUTOKUJUA USAHIHI WA KILE KINACHOMSUMBUA

Mara nyingi Binadam usumbuliwa na fikra zake kwa kufikiri kwa kina juu ya taarifa anayoipata, taarifa hizi huwa ni vichocheo katika  uchakatwaji wa taarifa ili kupata majibu yanayostahili.

Lakini ikumbukwe kuwa matokeo ya uchakatwaji wa taarifa unaendana na uelewa wa mhusika. Wagonjwa walio wengi uamini dalili zinazojitokeza wazi wazi kwenye miili yao  kwa mfano, kuumwa kichwa, kuwashwa mwili, kuumwa tumbo, n.k. Wakiamini ya kwamba dalili hizi zinatokana na ugonjwa fulani, La asha! Bali dalili hizi zitakuwa sahihi iwapo zitakuwa zimepata uthibitisho wa mtaalamu wa afya kwa kuwa anauelewa zaidi kuhusiana na magonjwa.

Wataalamu wa afya wamesomea dalili na visibitisho vya utambuzi wa magonjwa katika taasisi zinazoaminika pia  wanauzoefu unaotosheleza kubaini uhalisia wa ugonjwa.

Kwa ujumla chanzo cha taarifa za magonjwa ni katika jamii pamoja na wataalamu wa afya, Sisi wataalamu wa afya utapotupatia taarifa zenye vielelezo vya ugonjwa tutazichukua na kuzifanyia uchunguzi wa kina na kubainisha ugonjwa na matibabu  yake kulingana na kile kinachokusumbua.

Magonjwa yanayorudia mara kwa mara katika maeneo fulani yanawapa wataalamu wa afya uzoefu wa kubaini kwa urahisi magonjwa na matibabuyake. 

Wengi wa wagonjwa wanaoumwa kwa kile walichokuwa wanakiamini awali, sisi jukumu letu ni kurekebisha mtazamo wa mgonjwa kwa kile anachokiamini ambacho  sio sahihi, kwani hicho ndicho kinachopelekea ugonjwa wake usipate tiba sahihi.

Kwa maelezo zaidi kuhusu Dawa za mfumo mpya wa PHVs wasiliana nasi kwa simu namba +255782660707 au +255624066387 au WhatsApp +25578266070.

Neno la leo; Ishi kwa kutafakari.

No comments:

Post a Comment

TUJIKUMBUSHE TUMETOKA WAPI NA HIVI SASA TUPO WAPI

Mwaka 1983; Bukoba, Ugonjwa HIV/AIDS umeshititi miongoni mwa watu wazima na kuacha watoto wadogo yatima, wakazi wa vijijini waanza kukimbia ...