Asilimia kubwa ya watu katika jamii wanaokumbwa na tatizo la msongo wa mawazo hushindwa kuhimili kutokana na muingiliano wa taarifa anazozipata kutoka mwilini. Kwa mfano amepimwa shinikizo la damu akakutwa na presha ya juu, tokea hapo chochote kitakachomsumbua mwilini yeye udhani ni shinikizo la damu limepanda, hizi fikra zinasababisha kutokutambulika tatizo hasa linalomsumbua, kwani mshtuko wowote unaotokana na fikra husababisha shinikizo la damu kuwa juu, na kupoteza uhalisia wa tatizo.
Wakati mwingine mwili unapopata tatizo unaleta taarifa za kawaida pamoja na za hitilafu mwilini, na hizo taarifa za kawaida zinawezekana zikawa kwa muhusika ni mara ya kwanza kumtokea kwa hiyo zinamchanganya kifikra na kudhani ni tatizo na kusababisha ongezeko la msongo wa mawazo ambao unaleta mwilini matatizo mengi.
Msongo wa mawazo unachakatwa na tafsiri kutoka kwenye ubongo ambao unasimamia mambo kadha wa kadha mwilini, na iwapo msongo wa mawazo umeshititi mwili hukosa muelekeo na kuanzishwa magonjwa ya aina mbali mbali mwilini.
Msongo wa mawazo unasababisha wagonjwa wengi kutopona matatizo yao, iwapo hautopata matibabu yaliyokuwa sahihi.
Kwa maelezo zaidi kuhusu magonjwa ya binadamu na dawa za mfumo wa PHVs wasiliana nasi kwa simu namba +255782660707 au +255624066387 au whatsApp +255782660707
Neno la leo; Kujifunza ni lazima ikiwa unahitaji maisha bora.
No comments:
Post a Comment